1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya kuna uhaba wa dawa ya kuua Nzige

Admin.WagnerD28 Januari 2020

Serikali ya Kenya inakabiliwa na uhaba wa dawa za kunyunyiza nzige wa jangwani ambao wanaendelea kusambaa kwenye maeneo kadhaa,

https://p.dw.com/p/3WuX3
Somalia Heuschreckenplage Bauern
Picha: Reuters/F. Omar

Hayo yanajiri huku wataalam wakishauri kuanza kutumia ndege zisizokuwa na rubani kunyunyizia dawa ili kuongeza ufanisi dhidi ya nzige hayo wanaokaribia mji mkuu wa Nairobi.

Kwa mujibu wa waziri wa kilimo Peter Munya, uhaba huo wa dawa za kunyunyuzia nzige umesababishwa na urasimu uliopo kwenye mfumo mzima wa ununuzi, na kasi kubwa ya kusambaa kwa nzige hao.

Kwa sasa serikali inatumia kemikali aina ya Fenitrothion na Malathion kuwanyunyizia nzige hao wa jangwani.Dawa hiyo inanunuliwa kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo la FAO.

FAO yaonya kuhusu dawa za kuua wadudu hao

Heuschreckenplage in Ostafrika
Picha: Reuters/N. Mwangi

Hata hivyo baadhi ya maafisa wa FAO wametahadharisha kuwa huenda dawa hizo zikasababisha madhara kwani moja ya kemikali inayotumika imepigwa marufuku barani Ulaya.

Kemikali hiyo inaaminika kuwa na athari kwenye mazingira ukizingantia mfumo wa chakula, nyuki na viumbe vya majini.

Kwa sasa,maafisa wa FAO wanashauri matumizi ya dawa hiyo kwa vipimo vidogo.

Wiki iliyopita hazina maalum ya masuala ya dharura ya Umoja wa Mataifa iliridhia kuipa FAO shilingi bilioni 1.3 kununulia dawa za ziada ili kuimarisha operesheni za kunyunyiza.

Nzige wa jangwani wavamia baadhi ya maeneo nchini Kenya

Fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya mataifa ya Kenya, Ethiopia na Somalia yanayoshambuliwa zaidi na nzige. FAO iliomba shilingi bilioni 7 kwa jumla.

Ndege zisizo na rubani ni muhimu

Yote hayo yakiendelea wataalam nchini Kenya wanashauri matumizi ya ndege zisizokuwa na rubani ili kuongeza kasi ya kunyunyiza dawa ya kupambana na nzige wanaovamia maeneo ya milimani na mabondeni.

Wakulima nao wameingiwa na wasiwasi kwani nzige hao wanayakaribia maeneo ya kilimo.

Mwanzoni mwa wiki hii, shirika la kupambana na nzige katika ukanda wa mashariki liliweka bayana kuwa ndege zinazotumika kunyunyizia dawa nzige hao imeongezwa hadi 6.

Nzige hao wanaripotiwa kuvamia kaunti zipatazo 10 kwa sasa.TM,DW Nairobi.