KAMPALA : Maskini kupatiwa dola 6 | Habari za Ulimwengu | DW | 10.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KAMPALA : Maskini kupatiwa dola 6

Uganda italipa masurufu ya dola sita kwa mwezi kwa watu wanaoishi kwenye umasikini kwa muda mrefu nchini humo ambao wanaishi kwa kutegemea pungufu ya dola moja kwa siku.

Mpango huo wa dola milioni saba nukta saba unagharimiwa na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza na mashirika ya misadaa likiwemo shirika la Kimataifa la HelpAge.Dola nyengine sita zitakuwa zikitolewa kwa familia ambazo zinaangalia wazee, walemavu au mayatima.

Kwa mujibu wa serikali zaidi ya asilimia 25 ya watu milioni 30 wa Uganda ni maskini waliotopea.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com