1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Kaburi la halaiki la miongo kadhaa lafukuliwa Afghanistan

Sudi Mnette
13 Februari 2024

Maafisa nchini Afghanistan wanasema kaburi la pamoja lililokuwa na takriban miili 100 inayoaminika kuwa ya toka enzi kisovieti limegunduliwa katika mkoa wa Khost mashariki mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4cKmA
Viongozi wa vuguvugu la Taliban wakiwa mjini Moscow
Viongozi wa harakati ya Taliban wakitembea kuhudhuria mkutano na waandishi wa habari huko Moscow Julai 9, 2021Picha: Dimitar Dilkoff/AFP

Meya wa mkoa wa Khost, Bismillah Bilal amesema kaburi hilo limegunduliwa Jumamosi wakati wa ujenzi wa bwawa dogo katika eneo la Sarbani la Khost ya kati.Ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kwamba kwa mujibu wa taarifa za awali, watu hao walizikwa katika eneo hilo baada ya kuuawa mwaka 1358, kwa zingatio la  kalenda ya Afghanistan, inayolingana na Aprili 1979 hadi Machi 1980.Wakazi wa eneo hilo walisema mabaki hayo ni ya waathiriwa wa ghasia zilizofuatia mapinduzi ya kikomunisti yaliyoungwa mkono na utawala wa Kisovieti mwaka 1978 nchini Afghanistan.