KABUL: Taliban wamwachia huru mfaransa. | Habari za Ulimwengu | DW | 12.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Taliban wamwachia huru mfaransa.

Wanamgambo wa Taliban wamesema wamemwachia huru mfanyikazi wa kutoa misaada raia wa Ufaransa aliyetekwa kiasi wiki tano zilizopita katika eneo la kusini mwa Afghanistan.

Shirika la Msalaba Mwekundu limethibitisha Eric Damfreville, anayelifanyia kazi shirika la Terre d´Enfance, aliachiwa huru katika mkoa wa Kandahar.

Eric Damfreville na mwenzake raia wa kike wa Ufaransa pamoja na raia watatu wa Afghanistan walitekwa nyara tarehe tatu mwezi uliopita katika mkoa wa Nimroz kusini magharibi mwa Afghanistan.

Raia huyo wa kike wa Ufaransa aliachiwa huru wiki mbili zilizopita ingawa hatma ya mateka waliobaki haijulikani.

Wanamgambo wa Taliban walikuwa wameitaka Ufaransa kuondoa wanajeshi wake kiasi elfu moja nchini Afghanistan ili mateka hao waachiwe huru.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com