1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jung ataka katiba ibadilishwe

Oumilkher Hamidou10 Agosti 2009

Kampeni ya uchaguzi mkuu yapamba moto

https://p.dw.com/p/J6w1
Meli "Hansa Stavanger" baada ya kuachiliwa na maharamia wa kisomaliPicha: picture-alliance / dpa

Pendekezo la waziri wa ulinzi Franz Josef Jung kutaka jeshi la shirikisho liwe na uwezo mkubwa zaidi katika shughuli zake nchi za nje,wanamgambo wa ETA nchini Hispania wakiuka mipaka na chama cha SPD chazidi kudhoofika kutokana na kisa cha waziri wa afya Ulla Schmidt cha kutumia gari la serikali akiwa likizoni ndiozo mada zilizocha mbuliwa zaidi na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Tuenze lakini na jeshi la shirikisho Bundeswehr ambalo waziri wa ulinzi Franz Josef Jung anapendekeza lizidishiwe nguvu.Gazeti la STUTTGARTER NACHRICHTEN linaandika.

Baada ya miezi kadhaa ya kusumbuliwa kama mateka wa maharamia wa kisomali,mabaharia jasiri wa meli ya kijerumani "Hansa Stavanger" wamewasili katika bandari salama ya Mombasa.Katika wakati ambapo picha za kuachiliwa kwao huru zinaizunguka dunia,waziri wa ulinzi Franz Josef Jung anapigania katiba ifanyiwe marekebisho kwa namna ambayo kikosi maalum cha jeshi la shirikisho kiweze kuingilia kati nchi za nje kuwakomboa mahabusi.Anachokilenga hapo ni kimoja tuu nacho ni kwamba ikiwa katiba itaruhusu jambo kama hilo lifanyike nchi za nje,basi hata ndani jeshi la shirikisho Bundeswehr halitakua tena na pingamizi.Pengine wanasiasa wanalizusha suala hilo la katiba kwasababu wanatambua fika kikosi maalum kama hicho hakipo kabisa humu nchini.

Gazeti la SCHWÄBISCHE ZEITUNG linajiuliza:

"Amekusudia nini hasa waziri Jung?Ndo kusema anataka kuwatwika SPD makosa ya matukio dhaifu ya shughuli za jeshi la shirikisho katika kupambana na maharamia au vipi?Kwa hayo hatofanikiwa.Wasocial Democrat wanapinga mapendekezo ya kupanuliwa shughuli za jeshi la shirikisho ndani nchini sawa na wanavyopinga pendekezo la kugeuzwa Bundeswehr kuwa polisi ya dunia.Lakini wana SPD hawana pingamizi ikiwa jeshi la shirikisho litatumikia juhudi za Umoja wa Ulaya za kupambana na maharamia.Pendekezo la Franz Josef Jung lakini linatatanisha.

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha pia na mashambulio ya kigaidi ya wanamgambo wanaopigania kujitenga kwa jimbo la Bask la Hispania ETA.Gazeti la SÜDKURIER linaandika:

Kundi la magaidi la ETA laonyesha kubadilisha mkakati.Katika miaka ya nyuma mara nyingi walikua wakishambulia maeneo ya kaskazini ya Hispania tuu.Lakini wamepoteza imani ya wakaazi wa eneo hilo hivi sasa.Kila kwa mara wananchi wamekua wakiandamana kudai matumizi ya nguvu yakome.Hivi sasa wanamgambo wa ETA wanaonyesha kulenga shabaha mpya:Shughuli za utalii.Mabomu dhidi ya Mallorca ni sawa na miba ya mchongoma dhidi ya Hispania.Hata hivyo mbinu zao zimesalia pale pale;Kabla ya mabomu kuripuka,magaidi wa ETA wanaonya kwa simu.ETA hawataki kuuwa raia wala watalii,wanachokitaka ni kueneza hofu na wasi wasi .

Bundesgesundheitsministerin Ulla Schmidt
Waziri wa afya Ulla SchmidtPicha: AP

Mada yetu ya mwisho magazetin i hii leo inahusu kisa cha waziri wa afya Ulla Schmidt na chama chake cha SPD.Gazeti la NEUE OSNABRÜCKER ZEITUNG" linaandika.

Ulla Schmidt ataendelea kua mzigo kwa chama cha SPD.Kwasababu kila atakapojitokeza katika kampeni ya uchaguzi,nayo kadhia ya gari la serikali itazidi kuchomoza.Mgombea wa kiti cha kansela wa SPD,Frank-Walter Steinmeier anamsifu na kumtaja shujaa asiyewaogopa wenye maguvu.Tatizo la Ulla Schmidt lakini halikutikani katika kutumia gari la serikali.Kishindo kinakutikana katika siasa yake:Jinsi ya kutia njiani fuko linalobishwa la kugharimia huduma za afya, na jinsi madaktari walivyofungika bila ya wagonjwa kufaidika.