1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Julia Assange aruhusiwa kukata rufaa Uingereza

Saumu Mwasimba
24 Januari 2022

Muasisi wa mtandao wa kufichua siri wa WikiLeaks Julian Assange amefanikiwa katika ombi lake la kutaka  kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi ya Uingereza kupinga hatua ya kumrudisha Marekani

https://p.dw.com/p/460ft
Großbritannien | Protest gegen die Auslieferung von Julian Assange in London
Picha: Peter Nicholls/REUTERS

Mahakama kuu mjini London leo imempa haki mfichuzi huyo wa nyaraka za siri za Marekani ya kwenda kukata rufaa ya kuupinga uamuzi wake wa mwanzo uliotaka mwasisi huyo wa Wiki Leaks akabidhiwe kwa Marekani.

Rafiki wa Assange Stella Moris baada ya uamuzi huo aliseam kilichotokea mahakamani  ndicho walichokitarajia. 

"Kilichotokea mahakamani leo ndicho haswa tulichotaka kitokee. Mahakama kuu imejiridhisha kwamba tuliibua hoja ya kisheria yenye umuhimu kwa uma kwa ujumla na kuona kwamba mahakama ya juu zaidi ina sababu nzuri za kusikiliza rufaa hii,'' alisema Stella Moris.

soma zaidi: Hatma ya Assange kuamuliwa Uingereza

Mahakama ya chini ya Uingereza awali ilitowa uamuzi wa kukataa kumkabidhi Assange kwa Marekani ikisema Assange huenda akajiua akipelekwa katika mazingira magumu ya jela nchini Marekani.

Mahakama ya juu lakini mwezi uliopita iliubatilisha uamuzi huo wa mahakama ya chini,ikisema ahadi zilizotolewa na Marekani zinatosha kuhakikisha Assange hatojidhuru katika jela za Marekani.