Jonas Hector wa Cologne ajiunga na timu ya taifa | Michezo | DW | 07.11.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Jonas Hector wa Cologne ajiunga na timu ya taifa

Kocha wa Ujerumani Joachim Loew amemwita kikosini beki wa Cologne Jonas Hector kwa mara ya kwanza kabisa kwa ajili ya mechi zijazo dhidi ya Gibraltar na Uhispania

Hector mwenye umri wa miaka 24, ndilo jina la kushangaza kabisa katika kikosi cha Loew ambacho pia kinamjumuisha mshambuliaji wa Hoffenheim Kevin Volland, ambaye yiko kikosini kwa mara ya kwanza kucheza mchuano wa ushindani. Loew amesema anataka kumfahamu vyema Jonas Hector ambaye kwa sasa yuko katika kiwango kizuri cha mchezo wake katika klabu ya Cologne.

Wengine waliorejea katika kikosi hicho chenye wachezaji 23, ni beki Benedikt Hoewedes, na viungo Marco Reus, Sami Khedira na Lars Bender, ambao wamekuwa nje kwa ajili ya majeraha. Beki Mats Hummels na mshambuliaji Julian Draxler wako nje kwa ajili ya majeraha.

Hakukuwa na nafasi ya mshambuliaji Mario Gomez na kiungo Kevin Grosskreutz. Ujerumani itachuana na Gibraltar siku ya Ijumaa mjini Nuremberg katika mchuano wa kufuzu dimba la Mataifa ya Bara Ulaya Euro 2016 kabla ya kusafiri kuchuana na mabingwa wa ulimwengu na Ulaya Uhispania siku nne baadaye.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu