John Kerry kuzuru mashariki ya kati na Afrika | Matukio ya Kisiasa | DW | 18.05.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

John Kerry kuzuru mashariki ya kati na Afrika

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry anatarajiwa kusafiri kwenda katika mataifa ya mashariki ya kati na Afrika kuanzia Jumanne ijayo kwa ziara itakayomchukua hadi Mei 27.

US Secretary of State John Kerry exits his government aircraft (Foto: Reuters) / Eingestellt von wa

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry

Kerry anatarajiwa kuanza ziara yake mjini Muscat siku ya Jumanne (21.05.2013), ikifuatiwa na Jordan siku ya Jumatano, ambako atakutana na kile kinachoitwa "washirika muhimu wa kimataifa", kuangalia uwezekano wa kupatikana kwa suluhisho la kisiasa kupitia majadiliano nchini Syria , wizara ya mambo ya kigeni nchini Marekani imesema katika taarifa.

Mkutano huo unakuja kabla ya mkutano mkubwa wa kimataifa kuhusu Syria unaopangwa na Urusi na Marekani , na ambao unatarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Russian President Vladimir Putin (R) and the US Secretary of State John Kerry (L) hold talks in the Kremlin in Moscow on May 7, 2013. Kerry sought today to narrow differences over the conflict in Syria with Putin, urging the Russian strongman to find common ground to help end the bloodshed. AFP PHOTO/POOL/MLADEN ANTONOV (Photo credit should read MLADEN ANTONOV/AFP/Getty Images)

Kerry akiwa katika majadiliano na rais Putin wa Urusi

Siku ya Alhamis na Ijumaa , Kerry anatarajiwa kuzuru Jerusalem na Ramallah kufuatilia mazungumzo juu ya kuleta pamoja Israel na Palestina katika meza ya majadiliano, kujadili amani, taarifa hiyo imesema.

Sherehe za Umoja wa Afrika

Pia siku ya Ijumaa , Kerry anatarajiwa kusafiri kwenda mjini Addis Ababa kushiriki katika sherehe za siku mbili za kuadhimisha miaka 50 tangu kuundwa kwa Umoja wa nchi za Afrika OAU, ambao hivi sasa unajulikana kama Umoja wa Afrika, AU. viongozi kutoka sehemu mbali mbali za Afrika watahudhuria sherehe hizo.

Hapo Mei 26 , waziri Kerry anapanga kurejea mjini Amman Jordan kushiriki katika jukwaa la kiuchumi la dunia.

Wakati huo huo baraza la usalama la umoja wa mataifa linatafakari ombi kutoka kwa maafisa wa ngazi ya juu wa shirika la misaada la umoja huo linalodai kufikishwa kwa misaada katika nchi iliyoharibiwa kwa vita ya syria, hatua ambayo inaweza kusababisha hali ya mivutano baina ya Urusi na mataifa ya magharibi kuhusiana na upelekaji wa misaada ya kiutu kupitia mipakani, wamesema wanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa.

Members of the United Nations Security Council listen to Syria's U.N. Ambassador Bashar Ja'afari during a Security Council meeting on the situation in Syria at United Nations headquarters Thursday, July 19, 2012. Russia and China vetoed a U.N. resolution to imposes non-military sanctions on Syria. (AP Photo/Kathy Willens)

Baraza la usalama la umoja wa mataifa

Wakimbizi wamiminika nchi jirani

Wakati nchi jirani za Jordan, Lebanon, Uturuki na Iraq zinasumbuka kuhimili wimbi la wakimbizi wanaoingia katika nchi zao , ambao shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR, limesema siku ya Ijumaa, (17.05.2013), imevuka idadi ya watu milioni 1.5, maafisa wa umoja huo wameliambia baraza la usalama , kuwa kuna mamilioni ya watu wanaohitaji misaada ndani ya Syria.

Lakini mpambano wa aina hiyo kuhusiana na azimio jipya katika baraza hilo lenye wajumbe 15, ambalo kwa muda mrefu limeendelea kukwama kuhusiana na vipi wanaweza kuushughulikia mzozo wa Syria uliodumu miaka miwili sasa, huenda likaachwa hadi baada ya mkutano wa kimataifa kuhusu Syria utakaofanyika mjini geneva mwezi ujao, wameeleza wanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa.

Syria's President Bashar al-Assad speaks at the Opera House in Damascus in this still image taken from video January 6, 2013. REUTERS/Syrian TV via Reuters TV (SYRIA - Tags: POLITICS PROFILE TPX IMAGES OF THE DAY) NO SALES. NO ARCHIVES. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. IT IS DISTRIBUTED, EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS. SYRIA OUT. NO COMMERCIAL OR EDITORIAL SALES IN SYRIA

Bashar al-Assad akihutubia kwa njia ya Televisheni

Urusi, mshirika wa karibu wa rais wa Syria Bashar al-Assad na China zimetumia kura ya turufu mata tatu kuzuwia baraza hilo kuchukua hatua dhidi ya Assad, hatua zilizoungwa mkono na mataifa mengine matatu yenye kura hiyo, Marekani, Ufaransa na Uingereza.

Viongozi wa mataifa ya magharibi wamechukua tahadhari kuhusu uwezekano wa mafanikio ya mkutano wa syria mjini Geneva kuwa unaweza kupata kufikia kuondoa mkwamo, na mapendekezo ya Urusi kuwa Iran ni lazima ihudhurie katika mazungumzo hayo yameanza kufanya mambo kuwa magumu.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / dpae

Mhariri: Caro Robi

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com