1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yamuua kijana wa Kipalestina Ukingo wa Magaharibi

16 Novemba 2025

Jeshi la Israel limesema leo kuwa limemuua mtu mmoja katika oparesheni yake ya usiku kucha kwenye mji wa Nablus, katika eneo la Ukingo wa Magharibi.

https://p.dw.com/p/53iFY
Wapalestina katika eneo la Ukingo wa Magharibi.
Wapalestina katika eneo la Ukingo wa Magharibi wakitazama mashambulizi ya Israel yalivyoharibu makaazi yao.Picha: Mamoun Wazwaz/SIPA/picture alliance

Katika taarifa yake iliyotolewa mapema leo Israel imesema wakiwa katika oparesheni mtu mmoja alivurumisha kifaa cha mripuko kuelekea upande wa wanajeshi wake, nao wakamuua mtu huyo. Israel imesema hakukuwa na madhara kwa upande wake.

Wizara ya afya Palestina imethibitisha juu ya kifo cha kijana huyo mwenye umri wa miaka 19, ikisema aliuwawa katika kambi ya wakimbizi ya Askar baada ya kushambuliwa majira ya usiku.

Ukingo wa Magharibi umeendelea kushuhudia ongezeko la ghasia, tangu shambulio la Hamas dhidi ya Israel mnamo Oktoba 2023, ambapo zaidi ya Wapalestina 1,000 na Waisraeli 43 wameuawa katika mashambulizi kwenye eneo hilo.