JERUSALEM:Israel yadai Hezbollah yajiimarisha kisilaha | Habari za Ulimwengu | DW | 01.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM:Israel yadai Hezbollah yajiimarisha kisilaha

Israel imedai kwamba wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon wamejizatiti upya kisilaha na wanamiliki roketi zenye uwezo wa kupiga hadi ndani ya mji wa Tel Aviv na pia wameongeza mara tatu makombora yake aina ya C-802 yenye uwezo mkubwa.

Madai hayo ya Israel yametolewa katika ripoti ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Kin Moon ingawa Israel haijatoa ushahidi wowote wa kijasusi.

Hata hivyo katibu mkuu wa Umoja wa mataifa amesema hotuba za miezi ya hivi karibuni za kiongozi wa kundi hilo la Hezbollah Hassan Nasrallah zinaelekea kuthibitisha ukweli wa madai ya Israel.

Aidha katibu mkuu Ban Ki Moon amesema kujiimarisha kisilaha kwa kundi hilo la Hezbollah tangu vita vya mwaka na Israel kunazusha mashaka makubwa juu ya utekelezwaji wa azimio la Umoja wa mataifa lililomaliza vita hivyo vilivyochukua muda wa 34.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com