1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, Taliban ni kina nani?

18 Agosti 2021

Kundi la wapiganaji wa Kiisilamu limechukua madaraka tena nchini Afghanistan. Je, kundi la Taliban ni kina nani hasa na nini unahitaji kujua juu ya muundo wa uongozi wa Taliban

https://p.dw.com/p/3z7Hs
Afghanistan PK der Taliban
Picha: Stringer/REUTERS

Historia yao na nini cha kutarajia kutoka kwa utawala wao mpya. Mwandishi wa DW Carla Bleiker amelifafanua kundi hilo.

Wanajiita "wanafunzi" hiyo ndiyo tafsiri ya neno "Taliban" kutoka lugha ya Afghanistan ya pashto. Leo hii jina la vuguvugu la wapiganaji wa Kiisilamu haileti picha za wanaume na wanawake walioinama wakisoma vitabu, badala yake linadhihirisha ugaidi na uharibifu. Soma Licha ya ahadi ya Taliban kutolipiza kisasi, maelfu waondoka

Baada ya Taliban kumaliza kuchukua udhibiti nchini Afghanistan siku ya Jumapili kwa kuuteka mji mkuu Kabul na kuhamia ikulu ya rais, mamia ya raia waliuvamia uwanja wa ndege wa Kabul kwa hofu. Walijaribu kuingia kwenye ndege chache za kijeshi ambazo zilikuwa zimeanza kuruka, wakiwa na hamu kubwa ya kutoroka nchi ambayo sasa iko tena chini ya utawala wa Taliban. Soma Juhudi za kimataifa za kuwahamisha watu kutoka Afghanistan zashika kasi

Mfumo wa uongozi 

Usbekistan Taschkent | Ankunft Evakuierungsflug aus Kabul
Picha: Bundeswehr

Kuna mfumo wazi juu ya uongozi ndani ya kundi la Taliban. Mawlawi Hibatullah Akhundzada amekuwa kiongozi mkuu wa kundi hilo tangu 2016. Msomi huyo wa kidini ndiye mwenye mamlaka kuu katika masuala yote ya kisiasa, dini na kijeshi. Anaungwa mkono na manaibu watatu na mawaziri kadhaa ambao husimamia vitengo vya kijeshi, ujasusi na uchumi. "Rahbari Shura," anayejulikana pia kama "Quetta Shura," ndiye mwenye mamlaka ya juu zaidi ya ushauri wa kundi hilo lenye washirika 26.

Tawi la kisiasa la Taliban ambalo linaliwakilisha kundi hilo kimataifa liko mjini Doha, Qatar. Masuala ya siasa yanaongozwa na mwanzilishi mwenza wa Taliban Mullah Abdul Ghani Baradar. Hii ikiwa ni sehemu ndogo tu ya kundi la Taliban ambayo imeshughulikia mazungumzo ya amani na Marekani.

Wanapata wapi fedha za kujisimamia?

Afghanistan I Die Führung der Taliban
Picha: Sefa Karacan/AA/picture alliance

Kundi hili la wapiganaji linapata pesa nyingi kupitia usafirishaji wa mihadarati na dawa ya aina ya opium na heroin. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa mnamo 2018 na 2019 pekee, Taliban walipata zaidi ya dola milioni 400 kupitia biashara hii haramu ya dawa za kulevya, ambayo inachukua hadi asilimia 60 ya mapato ya kundi hilo.

Aidha ripoti ya Hanif Sufizada mchambuzi wa sera za uchumi katika kituo cha mafunzo cha Afghanistan amesema Taliban pia wana vyanzo vya ziada vya mapato ambavyo ni pamoja na madini, ushuru na michango. Inadhaniwa kuwa nchi nyengine pia hulifadhili kundi la Taliban kifedha.

Guido Steinberg, kutoka Taasisi ya Ujerumani ya Masuala ya Kimataifa na Usalama (SWP), aliiambia DW kwamba "Taliban wana washirika wawili, Mmoja ni mshirika asiyeonekana, Iran. Walinzi wa Mapinduzi wameunga mkono Taliban katika miaka ya hivi karibuni ili kuwashinda Wamarekani. Mshirika wao wa pili na muhimu zaidi ni Pakistan. Pakistan inapigana pamoja na Taliban."

Kundi la wapiganaji la Taliban liliibuka kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kikatili nchini Afghanistan ambavyo vilifuata kujiondoa kwa Umoja wa Kisovieti nchini humo na kundi hilo lilianzishwa rasmi mnamo 1994, wapiganaji wake wengi hapo awali walipigana dhidi ya vikosi vya Kisoviet vilivyokuwa vikidhibiti eneo hilo jaribio ambalo liliungwa mkono kwa siri na Shirika la ujasusi la Marekani CIA. Soma Umoja wa Mataifa wataka ulimwengu kuisaidia Afghanistan 

Sharia ya Kiislam

Mullah Mohammed Omar, ambaye angekuwa mwanzilishi wa Taliban, alivunjika moyo kwamba sheria ya Kiislamu haikuwekwa nchini Afghanistan baada ya kumalizika kwa uvamizi wa Kisoviet. Alikusanya wanafunzi 50 na kwa pamoja kundi hilo liliapa kuwaondoa wababe wa kivita na wahalifu, kurejesha utulivu, amani na usalama katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita.

Kikundi hicho kilikua kwa haraka, huku kikipata msaada kutoka Pakistan, na kuanza kuchukua miji na majimbo. Walikuwa maarufu kwa sababu walimaliza ufisadi na walifanya maeneo ambayo waliyadhibiti kuwa salama kwa biashara tena.

Mnamo 1996, walichukua udhibiti wa mji mkuu Kabul na kuipindua serikali. Kufikia 1998, serikali ya Taliban ilidhibiti asilimia 90 ya Afghanistan.

 

https://p.dw.com/p/3z3Xu