1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfahamu mgombea wa chama cha Kijani kumrithi Merkel

Thurau Jens Thomas Iddi Ssessanga
25 Agosti 2021

Annalena Baerbock anatajwa kuwa mkali, mwenye kipaji na mwenye tamaa ya kuendelea. Lakini tangu alipoteuliwa kugombea ukansela kupitia chama cha Kijani cha Ujeurmani, amekuwa akipambana kuzuwia mashambulizi ya mfululizo.

https://p.dw.com/p/3zTqO
Gremiensitzungen - Bündnis 90/Die Grünen | Annalena Baerbock
Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Annalena Baerbock alichaguliwa kuwa mgombea wa kwanza wa ukansela wa Chama cha Kijani mnamo Aprili, akisisitiza umoja ambao yeye na kiongozi mwenza Robert Habeck walifanya uamuzi, na kusudi lao la pamoja: Kuwa chama kipya kikubwa nchini Ujerumani.

"Kwa kweli hatukujua wakati huo kwamba tungekuwa tumesimama hapa leo," alisema mnamo mwezi Aprili. "Lakini tulichojua ni kwamba tunataka kutanua chama chetu, kwamba tunataka kutengeneza sera kwa ajili ya jamii pana: Chenye kuvutia, na chenye malengo yalio wazi. Na kwa hivyo leo unaanza ukurasa mpya kwa chama chetu."

"Hapa leo, nataka kutoa pendekezo, kwa jamii nzima, kama mwaliko wa kuongoza nchi yetu anuwai, yenye nguvu na tajiri kuelekea mustakabali mzuri," aliongeza wakati akijianda na mada hiyo.

Soma pia: Annalena Baerbock mgombea ukansela wa chama cha Kijani

Hapo awali, Baerbock - ambaye hajawahi kushika wadhifa wowote serikalini - alisifiwa kwa kuongezeka kwa umaarufu wa chama chake mwishoni mwa Aprili 2021.

Biesenthal | Baerbock und Habeck | Vorstellung Grünen-Pläne zu Klimaschutzministerium
Annalena Baercback akizungumza katika mkutano wa habari na kiongozi mwenza wa chama cha Kijani Robert Habeck.Picha: TOBIAS SCHWARZ/AFP

Lakini baadae alikabiliwa na mashabulizi yanayomlega yeye binafsi, na kufanya aanze kujitetea, kutokana na ukosoaji huo kulenga uaminifu wake wa binafsi: Alituhumiwa kwa makosa madogo katika wasifu wake rasmi, kwa kuchelewesha kulipa kodi ya bonasi kubwa ya Krismasi, kwa kutumia maandiko yasio yake katika baadhi ya sehemu za kitabu chake pasina kutaja wenye maandiko hayo, na kisha akatumia neno la ubaguzi wa rangi kwenye nukuu katika mahojiano. Kila wakati Baerbock alikuwa mwepesi kuomba msamaha. Lakini viwango vya umaarufu wake vimeshuka.

Soma pia: CDU yamchagua Laschet kuwa mgombea wa ukansela

Baerbock mwenye umri wa miaka 40 aliibuka katika mkutano wa chama mapema 2018. Mwanasiasa huyo wa jimbo ambaye hakuwa anajulikana sana -- mkazi wa jimbo la Brandenburg -- alijitokeza mbele na kuwaahidi wajumbe ambao walikuwa wamemfanya kuwa mmoja wa viongozi wenza wa chama hicho.

Hatua ilikuwa na bado ni ya kushangaza. Kwa sababu wanamazingira tayari walikuwa na nyota moja tu: Mwanasiasa kijana Robert Habeck na ambaye kwa wengi alikuwa ametajwa kuwa mtu anayeweza kuwania ukansela.

Lakini tangu aingie kwenye nafasi ya mwenyekiti mwenza wa chama hicho, Baerbock amejitambulisha kama mtaalamu wa jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Pia amezungumzia masuala magumu ya sera ya kigeni. Na kuhusu vitisho vinavyosababishwa na siasa kali za mrengo wa kulia na chuki inayotokana na hofu dhidi ya wageni.

Soma pia: Warithi watarajiwa wa Merkel watofautiana kuhusu China, Urusi

Awali, Baerbock alisukumwa na malengo. Mzaliwa huyo wa mwaka 1980 katika mji mdogo wa Pattensen jimboni Lower Saxony, alikuwa na kipaji cha asili cha riadha, akishika nafasi ya tatu kitaifa katika mashindano ya kukanyaga ya Ujerumani. Alikuwa na miaka 16 tu alipokwenda kukaa kwa mwaka mmoja nchini Marekani.

Baadae, alisomea sheria mjini Hannover kabla ya kujiunga na chuo cha uchumi cha London, ambako alisomea sheria ya kimataifa. Matokeo yake, Baerbock anatoa mahojiano kwa Kiingereza fasaha -- jambo ambalo hadi katika wakati huu halichukuliwi kimzaha miongoni mwa wanasiasa wa Ujerumani.

Tangu awe kiongozi-mwenza wa chama, chama cha Kijani kimekua kikifanya vizuri kwenye uchunguzi wa maoni ya wapigakura, kikiwa na umaarufu wa zaidi ya asilimia 20. Hilo linajumlishwa pia na uwakilishi mzuri wa chama hicho katika bunge la Ulaya, na pia kura za majimbo nchini Ujerumani.

Wahlplakate Bundestagswahl 2021
Mabango ya kuwanadi wagombea yakiwa yamepamba mandhari katika mtaa mmoja wa Brandenburg.Picha: picture alliance / Jörg Carstensen

Lakini chama cha Kijani bado kinapambana na kuweka mizizi mashariki mwa Ujerumani. Baerbock na familia yake ya watu wanne wamekuwa na makao yao katika mji wa mashariki wa Potsdam, ambako anagombea dhidi ya mshindani kutoka chama cha Social Democratic kwa nafasi ya kansela, Olaf Scholz.

Uharakishaji wa usitishaji matumizi ya mafuta na udhibiti wa kasi barabarani

Baerbock na Habeck wana vizuizi vichache juu ya kuzungumza na wanachama wa vyama vingine, wakiwemo wahafidhina, kutafuta uwezekano wa msingi wa maelewano. Na kumekuwa na uvumi mwingi juu ya uwezekano wa muungano wa kihafidhina-Kijani mjini Berlin baada ya uchaguzi wa 2021.

Lakini Baerbock amefanya kazi kwa bidii kuelekea jukwaa la chama lililofafanuliwa vizuri, ambalo linatofautiana wazi wazi na sera za kambi ya wahafidhina. Kwa mfano, anataka kuona Ujerumani ikiondoa nishati inayotumia makaa ya mawe mapema zaidi kuliko shabaha ya sasa ya mwaka wa 2038.

Soma pia: Ujerumani Chama cha Kijani chaadhimisha miaka 40

Yeye pia anaunga mkono kikomo cha kasi cha kilomita 130 kwa saa (maili 80 kwa saa) kwenye "Autobahn," kama barabara kuu za Ujerumani zinavyojulikana. Yeye pia anapinga kupandishwa kwa bajeti ya matumizi ya ulinzi ya Ujerumani.

Hii inaacha nafasi ndogo ya mashaka kwamba uwezekano wowote wa muungano kati ya watetezi wa mazingira chini ya Baerbock na wahafidhina, utakuwa utaratibu tepetepe.

Deutschland | Wahlplakate in Oberhausen
Annalena Baerbock anajitanabahisha kama kiongozi mwenye mikakati ya kutatua changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.Picha: Revierfoto/dpa/picture alliance

Mpango wa Kijani wa kanda ya 'Atlantic'

Katika mahojiano na DW mwanzoni mwa 2021, Annalena Baerbock alikaribisha uamuzi wa Rais Joe Biden wa kuirudisha Marekani katika Mkataba wa Tabianchi wa Paris. Lakini kiongozi huyo mwenza wa chama cha Kijani pia aliainisha malengo yake thabiti na ya wazi kuhusu tabianchi.

"Sisi Waulaya, ikiwemo serikali ya Ujerumani, tunahitaji kutumia fursa ya hali ya sasa kutekeleza mapendekezo ambayo serikali ya Marekani imetoa juu ya ushirikiano kuhusu tabianchi. Tunahitaji kusonga na kuelekeza njia kuelekea Mpango wa Kijani wa Ulaya na Amerika."

Soma pia: Je chama cha Kijani Ujerumani ni chama kipya cha umma?

Katika ilani yao ya uchaguzi, Greens hawajawahi - kama ilivyokuwa mara nyingi huko nyuma - walionyesha upendeleo kwa muungano unaosimamia na Wanademokrasia wa Jamii wa kushoto (SPD). Kwa vyovyote vile, muungano wowote labda utahitaji ushiriki wa mtu wa tatu kufikia wengi, na soko la bure la libertarian Democrats Bure mgombea anayewezekana.

Katika ilani yao ya uchaguzi, chama cha Kijani hakijatangaza -- kama ambavyo imekuwa huko nyuma -- kwamba kinataka kuunda muungano na chama cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto cha Social Demcoratic SPD. Kwa vyovote vile, muungano wowote yumkini utahitaji ushiriki wa chama cha tatu ili kufikia wingi, ambapo chama cha kiliberali kinachoelemea biashara kikionekana kuwa mshirika mwenye uwezekano mkubwa.

Chanzo: DW

Mhariri: Daniel Gakuba