1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Japan kufanya linalowezekana ili kuzuia dharura za kiusalama

Hawa Bihoga
23 Machi 2024

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida amesema nchi hiyo itaimarisha uwezo wake wa ulinzi na Kidiplomasia ili kudumisha amani na kuongeza kuwa, uimara wa kijeshi umekuwa ukiongezeka.

https://p.dw.com/p/4e3Kv
Yokusuka, Japan | Wazirimkuu Fumio Kishida akiwa na maafisa wengine wa kijeshi
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida akiwa ameambatana na maafisa wengine wa kijeshiPicha: K. Narax/Future Image/IMAGO

Kishida amesema hayo katika hafla ya mahafali katika chuo cha Ulinzi wa Kitaifa mjini Yokusuka, na kuongeza kuwa Japan inakabiliwa na mazingira magumu na yenye changamoto nyingi za kiusalama tangu Vita vya Pili vya Dunia na kwamba serikali itafanya kila liwezekanalo ili kuzuia dharura za kiusalama.

Soma pia:Waziri Mkuu wa Japan aomba radhi kwa kashfa ya rushwa

Waziri Mkuu Kishida na Rais wa Marekani Joe Biden wanatarajiwa kufanya mkutano wa kilele Aprili 10 nchini Marekani, unaolenga kuimarisha uhusiano wa muda mrefu wa usalama wa nchi hizo mbili katika kukabiliana na ongezeko la ushawishi wa China na kitisho cha Korea Kaskazini inayoendelea na majaribio yake ya silaha nzito.