1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jamii za Herero na Nama zatafuta haki Namibia

Zainab Aziz
4 Machi 2024

Watu wa jamii za Herero na Nama nchini Namibia wanasema makubaliano yaliotiwa saini kati ya serikali yao na Ujerumani yamewadhihaki na wanataka haki.

https://p.dw.com/p/4d9sM
Berlin| Wawakilishi wa jamii za Herero na Nama
Wawakilishi wa jamii za Nama na HereroPicha: Abdulhamid Hosbas/AA/picture alliance

Baada ya kifo cha rais wa Namibia Hage Geingob, aliyekuwa mjumbe maalum wa Namibia kwenye mazungumzo na Ujerumani juu ya mauaji ya kimbari Dr. Zedekia Ngavirue, amesema watu wa jamii zilizoathirika wanataka makubaliano yaliyotiwa saini na Ujerumani mnamo mwaka 2021 yajadiliwe tena.

Soma pia: Ni lini Ujerumani itaiomba msamaha Namibia juu ya mauaji?

Watu hao wanataka wahusishwe zaidi kwenye mazungumzo, tofauti na mpangilio uliopo sasa. Jamii hizo zinaona kuwa makubaliano yaliyotiwa saini yamewadhihaki na kuwasaliti kwa sababu mapatano hayo hayakuzingatia swala la ardhi.

Hata baada ya kupita muda wa karne moja jamaa na ndugu walioathirika bado hawana ardhi kwa ajili ya kilimo. Ardhi yao iliporwa na wakoloni wa kijerumani na maalfu ya ekari yanaendelea kumilikiwa na vizazi vya walowezi hao wanaodai kuwa walinunua ardhi hiyo kwa njia halali nchini Namibia.