1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Namibia

Jamhuri ya Namibia ni nchi iliyoko kusini mwa Afrika, na koloni la zamani la Ujerumani. Ilipata uhuru wake kutoka Afrika Kusini mwaka 1990, kufuatia vita vya uhuru wa Namibia.

Mji Mkuu wa Namibia ambao pia ndiyo mji mkubwa zaidi ni Windhoek. Sehemu kubwa ya eneo lake ilikuwa inatawaliwa na Ujerumani mwaka 1884 na iliendelea kuwa koloni la Ujerumani hadi mwishoni mwa Vita Kuu ya kwanza ya Dunia. Afrika Kusini ilikalia koloni hilo mwaka 1915 na kulitawala kuanzia 1919 na kuendelea kama eneo la mamlaka ya Ligi ya Mataifa. Tangu ilipopata uhuru wake, Namibia imefanikiwa kukamilisha mpito wa kutoka utawala wa weupe wachache na kuunda demokrasia ya mfumo wa bunge.

Onesha makala zaidi