JAKARTA: Rais George W.Bush aitembelea Indonesia | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JAKARTA: Rais George W.Bush aitembelea Indonesia

Rais wa Marekani, George W. Bush amefanya ziara fupi lakini ya kutatanisha katika nchi ya Indonesia yenye waislamu wengi zaidi duniani. Usalama ulikuwa umeimarishwa vya kutosha. Maelfu kadhaa ya raia wamefanya maandamano katika mji mkuu Jakarta na miji mingine ya nchi, kuzipinga siasa za rais Bush hususan nchini Irak, Afghanistan na Mashariki ya kati. Rais Bush alikwenda nchini Indonesia akitokea Vietnam ambako alishiriki katika mkutano wa 21 wa jumuiya ya ushirikiano ya nchi za Asia na Pacifik, APEC. Viongozi kwenye mkutano huo, walikubaliana kuyainua mazungumzo ya Shirika la biashara duniani WTO yaliokwama. Taarifa ya pamoja ya kukamilisha mkutano huo, ilisema kuna hatari kubwa ikiwa mazungumzo ya WTO ya Doha yaliosimama tangu mwezi Julai, yatashindwa kabisa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com