1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yashambulia Gaza na kuamuru watu zaidi kuondoka Rafah

11 Mei 2024

Israel leo imeendeleza mashambulizi katika maeneo ya ukanda wa Gaza ikiwa ni pamoja na eneo la kusini mwa mji wa Rafah kusini.

https://p.dw.com/p/4fkAJ
Gaza inakabiliwa na ukosefu mkubwa wa maji
Hali ya kiutu imezidi kuwa mbaya Ukanda wa Gaza. Hayo ni kulingana na mashirika ya kimataifa. Picha: AFP

Israel pia imetoa amri ya watu kuhamia maeneo salama licha ya tahadhari ya Umoja wa Mataifa dhidi ya kushambulia eneo mji huo wa Rafah uliofurika watu.

Shirika la habari la Ufaransa AFP, madaktari na wengine walioshuhudia, wameripoti kutokea kwa mashambulizi katika eneo la pwani, ambapo Umoja wa Mataifa unasema misaada ya kibinadamu imezuiwa.

Hii ni baada ya wanajeshi hao wa Israel kukaidi wito wa kimataifa wa kutoishambulia Rafah na wiki hii kuingia katika eneo la mashariki mwa mji huo, hatua iliyosababisha kufungwa kwa kivuko kimoja muhimu cha msaada.

Taarifa ya hospitali ya Al-Aqsa Martyrs mjini Deir al-Balah, imesema kuwa takriban watu 21 waliuawa wakati wa mashambulizi katikakati mwa Gaza na kupelekwa hospitalini humo.

Mjini Rafah, mashuhuda wameripoti kuwepo kwa mashambulizi makali ya anga karibu na kivuko kinachopakana na Misri.

Mashambulizi mengine yanaripotiwa Kaskazini mwa Gaza.