1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fahamu jukumu la Baraza la vita Israel

18 Aprili 2024

Suali kubwa linaloulizwa baada ya Iran kuishambulia Israel ni namna Israel itakavyojibu mashambulizi hayo. Baraza la mawaziri linaloshughulikia masuala ya vita litakuwa na jukumu kubwa katika jibu la Telaviv kwa Tehran.

https://p.dw.com/p/4etQF
Israel Netanjahu, Galant na Gantz wakiwa mjini Tel Aviv
Baraza la vita la Israel likiongozwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu Picha: Abir Sultan via REUTERS

Iran na Israel zinashambuliana wakati dunia ikihofia kuwa mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati huenda ukatanuka zaidi. Siku ya Jumamosi Iran iliirushia Israel madroni 300 pamoja na kuifyetulia makombora  yaliyofanikiwa kudunguliwa kwa asilimia 99 na Israel.

Jamhuri hiyo ya kiislamu ya Iran imesema imefanya hivyo kujibu shambulizi lililodaiwa kufanywa na Israel katika ubalozi wake mdogo mjini Damascus, Syria lililosababisha mauaji ya makamanda wake saba mnamo Aprili mosi.

Israel yahimizwa kutojibu shambulizi la Iran

Peter Lintl, mtafiti katika taasisi ya Ujerumani inayoshughulikia masuala ya kimataifa na usalama, amesema jibu la Israel kwa Iran litaleta madhara makubwa zaidi katika ukanda mzima wa Mashariki ya Kati.

Lakini je nani anaamua kuhusu Israel kujibu au kutojibu mmashambulizi hayo?

Muda mfupi baada ya Kundi la wanamgambo wa Hamas kuvamia Kusini mwa Israel Oktoba saba na kusababisha vifo vya watu1,200 pamoja na kuwachukua mateka watu kadhaa, serikali ya Israel iliamua kuunda Baraza la mawaziri lililo na wanachama watatu litakaloshughulikia masuala ya vita. Baraza hilo linajukumu la kushughulikia operesheni za kijeshi ambazo Israel ilianzisha mjini Gaza kujibu shambulizi la Hamas.

Netanyahu asema Israel itajiamulia yenyewe masuala yake ya usalama

Maafisa wa Israel na Marekani wanasema kwamba Iran inaliunga mkono kundi la Hamas ambalo Marekani, Ujerumani na Umoja wa Ulaya zimeliorodhesha kundi hilo kama kundi la kigaidi. Iran pia inasemekana kulipa kundi hilo silaha pamoja na kuwapa mafunzo ya kijeshi, kwahiyo washirika wa Israel wanasema Iran kwa namna moja au nyengine ilihusika pia katika shambulio la Oktoba 7.

Baraza la vita linaongozwa na nani?

Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant (katikati) akihuzuria mkutano wa baraza la vita la Israel
Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant (katikati) akihuzuria mkutano wa baraza la vita la IsraelPicha: Israeli Ministry of Defense/Handout/Anadolu/picture alliance

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kutoka chama cha mrengo wa kulia cha Likud ndio anaeongoza Baraza hilo la masuala ya vita, Mawaziri wake wengine anaeshauriana nao pia wanatokea chama chake cha Likud, ambao ni Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant pamoja na aliyekuwa kiongozi wa upinzani Benny Gantz.

Viongozi wa dunia waihimiza Israel kutolipiza kisasi

Waangalizi wa Baraza hilo ni majenerali wastaafu watatu, jenerali Gadi Eisenkot wa chama cha National Unity, Aryeh Deri, kiongozi wa chama cha Shas chenye sera kali ya dini ya kiyahudi na waziri wa masuala ya kimkakati Ron Dermer. Wote wanaweza kuingia katika vikao vya baraza hilo lakini hawaruhusiwi kupiga kura au kufanya uamuzi wa aina yoyote.

Kwanini Israel ina serikali ya dharura?

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Nentanyahu aongoza baraza la vita la serikali yake
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Nentanyahu aongoza baraza la vita la serikali yakePicha: Ronen Zvulun/AFP/Getty Images

Kufuatia mashambulizi ya Oktoba 7, Baraza la Usalama la Israel liliiweka nchi chini ya hali ya vita na kuruhusu shughuli fulani za kijeshi kuanzishwa kujibu shambulizi la Hamas. Baraza la sasa hivi la Mawaziri Israel linachukuliwa kuwa na wafuasi wengi kutoka mrengo wa kulia kuwahi kushuhudiwa katika historia ya serikali za Israel. Lintl anaamini Baraza hilo la mawaziri limekamilika na linatosha kabisa kufanya maamuzi ya kisiasa na kijeshi juu ya operesheni za kijeshi katika ukanda wa Gaza.

Guterres: Mashariki ya Kati iko katika ukingo wa vita

Kuhusu Iran, mashambulizi iliyofanya Israel na majibu ya Israel kwa Iran Lintl  amesema Israel huenda ikashambulia lakini suali ni lini, wapi na vipi. Kufuatia shambulizi la Iran la siku ya Jumamosi Baraza hilo la mawaziri linaloshughulikia masuala ya vita la Israel lilikutana mara tatu kujadili majibu yake kwa taifa hilo la Iran.

Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na washirika wa Israel wa nchi za Magharibi ikiwemo Marekani, Uingereza  na Ufaransa wamekuwa wakiitolea mwito Israel kujizuwia ili kuepuka kuutanua mzozo ulioko kuwa mgogoro wa kanda nzima.

Baerbock ziarani Israel tena kusaka suluhisho la mgogoro