1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel: Wapatanishi waendelee na juhudi za kuwaokoa mateka

23 Mei 2024

Baraza la mawaziri la vita la Israel limewahimiza wapatanishi kuendeleza juhudi za kuachiwa huru kwa mateka wanaoshikiliwa na kundi la wanamgambo la Hamas.

https://p.dw.com/p/4gCC9
Baadhi ya mateka waliookolewa na jeshi la Israel
Baadhi ya mateka waliookolewa na jeshi la IsraelPicha: Israeli Army/AP/picture alliance

Baraza la mawaziri la vita la Israel limewahimiza wapatanishi kuendeleza juhudi za kuachiwa huru kwa mateka wanaoshikiliwa na kundi la wanamgambo la Hamas.

Haya yameripotiwa mapema leo na vyombo vya habari vya Israel vikinukuu taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu.

Baraza hilo la mawaziri la vita lilikutana awali kwa muda wa masaa manne.

Soma pia: Makombora ya anga ya Israel yauwa 35 Gaza

Israel na kundi la wanamgambo la Hamas, haziko katika mazungumzo ya moja kwa moja wakati Misri, Qatar na Marekani zikisimamia mazungumzo hayo ya amani kuhusu vita katika ukanda wa Gaza.

Duru ya mazungumzo ya hivi karibuni zaidi ilimalizika bila ya mafanikio yoyote. Tangu wakati huo, mazungumzo hayo yamekwama.

Katika mashambulizi ya kushtukiza yaliyofanywa na Hamas na makundi mengine ya itikadi kali katika mpaka wa Israel mnamo Oktoba mwaka jana, takriban watu 1200 waliuawa na wengine zaidi ya 200 kuchukuliwa mateka katika ukanda wa Gaza.