ISLAMABAD: Ripoti zatatanisha kuhusu Mullah Obaidullah Akhund | Habari za Ulimwengu | DW | 03.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Ripoti zatatanisha kuhusu Mullah Obaidullah Akhund

Ripoti zinasema,maafisa wa Pakistan na Marekani mjini Islamabad,wameanza kumhoji aliekuwa waziri wa ulinzi wa serikali ya zamani ya Wataliban. Inasemekana kwamba Mullah Obaidullah Akhund alikamatwa siku ya Jumatano pamoja na washukiwa wengine 4 katika mji wa Quetta,ulio kusini-magharibi ya Pakistan.Akhund anajulikana kama ni kiongozi muhimu katika mtandao wa Taliban na hivyo maafisa wa usalama wanatumaini kuwa ataweza kutoa habari kuhusu wanamgambo wengine walio muhimu.Serikali ya Pakistan bado haijathibitisha ikiwa kweli Mullah Obaidullah Akhund amekamatwa,lakini Wataliban wamekanusha ripoti hiyo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com