ISLAMABAD: Bin Laden atoa wito kumpindua Musharraf | Habari za Ulimwengu | DW | 21.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Bin Laden atoa wito kumpindua Musharraf

Kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda,Osama Bin Laden ametoa mwito kwa umma wa Pakistan kumpindua Rais Pervez Musharraf.Katika tepu mpya ya sauti,iliyotolewa kwenye mtandao wa Internet, Bin Laden amesema,ni wajibu wa Waislamu kuasi dhidi ya Musharraf ili kulipiza kisasi uvamizi wa Msikiti Mwekundu uliofanywa miezi miwili iliyopita mjini Islamabad.

Lakini msemaji wa majeshi ya Pakistan,amepuuza tangazo la Bin Laden na akaongezea kuwa vita dhidi ya al-Qaeda na wanamgambo wengine vitaendelea.Hapo awali,halmshauri ya uchaguzi ya Pakistan,ilitangaza kuwa uchaguzi wa rais utafanywa tarehe 6 mwezi wa Oktoba.Rais Musharraf alie mshirika mkuu wa Marekani kupiga vita ugaidi amesema,atagombea tena uchaguzi wa rais na wakati huo huo atabakia kama mkuu wa majeshi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com