Iran yatoa onyo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
3 Aprili 2026
Iran imelionya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya "hatua yoyote ya uchochezi", kabla ya kura iliyopangwa kuhusu rasimu ya azimio kuhusu Mlango-Bahari wa Hormuz ambayo hata hivyo imeahirishwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran,Abbas Araghchi alisema kitendo chochote cha uchochezi kinachofanywa na wavamizi na wafuasi wao, ikiwa ni pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali katika Mlango-Bahari wa Hormuz, kitasababisha hali mbaya zaidi.
Baraza hilo lenye wanachama 15 lilitarajiwa kupiga kura Ijumaa kuhusu rasimu ya azimio lililowasilishwa na Bahrain la kuruhusu mataifa kutumia nguvu kuhakikisha usafiri wa kimataifa unaendelea katika mlango bahari wa Hormuz. Tarehe mpya kuhusu kura hiyo bado haijatangazwa.
Mlango-Bahari wa Hormuz, njia muhimu ya meli inayopitisha nishati duniani, ulifungwa na Iran baada ya Marekanina Israel kuanzisha mashambulizi dhidi ya Iran mnamo Februari 28.