Iran Nyuklia | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 13.11.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Iran Nyuklia

Iran imetoa tarehe ya mkutano wa kujadili mpango wake wa nyuklia

default

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Margaret Ashton.

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton, amepokea ombi kutoka kwa mpatanishi mkuu wa masuala ya nyuklia wa Iran, Saeed Jalili,  la kukutana mapema mwezi ujao kujadili mpango wa nyuklia wa Iran. Wiki hii,Jalili alimuandikia Ashton barua kupendekeza  kukutana mjini Istanbul.Baada ya kushauriana na mataifa sita makuu duniani, yatakayowakilishwa na  Ashton yaani,  Marekani, Urusi, China, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani, kiongozi huyo amekubali kukutana tarehe 5 mwezi ujao wa Desemba  ikiwa utafanyika nchini Switzerland au Austria. Iwapo pande zote mbili zitakubaliana, hiyo itakuwa ni mara ya kwanza  kwa Iran kukutana kujadili mpango wake wa nyuklia baada ya zaidi ya mwaka mmoja.

Catherine Ashton Said Dschalili, Saeed Jalili Fotomontage Kombo

Catherine Ashton na mpatanishi mkuu wa masuala ya nyuklia wa Iran, Saeed Jalili.

Wapatanishi wa nchi za Magharibi wanasema hawana tatizo na Iran kumiliki kiwanda cha nyuklia kwa matumizi ya kiraia, lakini wanataka hakikisho kwamba mpango huo hautumiwi kurutubisha kwa siri madini ya Uranium hadi kiwango cha kuweza kutengeneza silaha za nyuklia.

Mwandishi Maryam Abdalla/Rtre/Afpe

Mhariri:Prema Martin

 • Tarehe 13.11.2010
 • Mwandishi Valvur, Andrus
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Q7gu
 • Tarehe 13.11.2010
 • Mwandishi Valvur, Andrus
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Q7gu

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com