Indonesia yasema wanajeshi 8000 wako tayari kupelekwa Gaza
15 Februari 2026
Matangazo
Kikosi cha jeshi la taifa la Indonesia, linalojulikana na kama TNI, kimekamilisha maandalizi ya vikosi vilivyopendekezwa pamoja na ratiba ya harakati zao kwenda Gaza ingawa bado serikali haijaamua ni lini wanajeshi hao watapelekwa. Haya ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi Brigedia Jenerali Donny Pramono.
Pramono ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba kimsingi, wako tayari kutumwa popote kwa notisi ya muda mfupi pindi serikali itakapoidhinisha rasmi.
Pia amesema, jeshi limetayarisha kikosi hicho cha takriban askari 8,000 kutokana na maamuzi yaliofanywa wakati wa mkutano wa Februari 12.