Ilikuaje hata Deutsche Bank kula nayo hasara ? | Magazetini | DW | 15.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Ilikuaje hata Deutsche Bank kula nayo hasara ?

Ni moja kati ya mada zilizochambuliwa :

Safu za leo za maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani, zimechambua zaidi mada 2:Mjadala wa jana Bungeni -Bundestag kuhusu mpango wa serikali ya Kanzela Angela Merkel wa kuutia jeki uchumi na juu ya hasara kubwa iiliopata banki maarufu ya Ujerumani : Deutsche Bank ya Euro bilioni 10 baina ya faida iliotia 2007 na ile ya mwaka jana 2008. Hata ari ya kufanya kazi ya wajerumani hivi sasa imezungumzwa:

Deutsche Bank.Gazeti la NEUE OSNABRUCKER ZEITUNG laandika:

"Kima hicho cha kasoro ya Euro bilioni 10 ilichopata DB ,ni sawa na mfuko mzima wa matumizi ya mwaka ya wizara mbili- ile ya fedha na ya uchumi.

Wakati huo huo Banki ya Posta (Post Bank), sasa inachukuliwa na DB. ....Je, hali ya mambo inazidi kuwa mbaya ? Hasara iliopata DB mwishoni mwa mwaka uliopita, imewasangaza wengi.Ni matokeo wazi ya kuachana na matawi yake yasiotia faida......hii yadhihirisha ,kifedha, DB ina pia kikomo chake.Lakini, kuonesha hali nyengine kipindi hiki cha misukosuko ingelikuwa ajabu."

Kwa kutangaza mkuu wa Deutsche Bank Bw.Josef Ackermann kuwa Banki yake imepatwa na hasara ya kwanza kubwa kabisa ya mabilioni tangu vita vya pili vya dunia,imani nyengine kwa mabenki inapotea....Gazeti linaongeza:

"Yafaa kuuliza lakini,kwanini mabenki nayo hayaachwi kufuata mkondo wa kujitangaza yamefilisika ? Kwani, kuna mabenki mengine yakutosha yanayoweza kuingilia kati na kuikoa benki iliofilisika. Hatari ya kujiingiza serikali na kuzidi kujitwika madeni ili kuyaokoa mabenki kutofilisika,sasa imekuwa kubwa.Kwani, madeni yote hayo inayobeba serikali ni malipo ya walipakodi wa kesho."

Nurnberger Nachrichten kuhusu Deutsche Bank linadai kwamba, wakati umewadia kwa mkuu wa Deutsche Bank kuungama kuwa msukosuko wsa fedha ulimwenguni pia umelikumba pia Banki yake.Hapo Deutsche Bank laandika gazeti-imepoteza nayo hadhi yake kuwa ni banki isioyumbishwa na misukosuko:

"Na hii si sifa njema kwa DB na hasa kwa tawi la taasisi za fedha lililokwisha poteza imani .Kila kukicha, balaa hili jinsi lilivyokubwa yazidi kudhihirika.Kuonesha hapa masikitiko hakusaidii kitu.Hatahivyo, DB inaendelea kudai haihitaji msaada wa serikali kujiokoa."

Gazeti la Emder Zeitung limefanya uchunguzi juu ya ari ya wafanyikazi ilivyo wakati huu makazini nchini Ujerumani na limegundua:

"Kuwa thuluthi mbili ya wafanyikazi wa Ujerumani hivi sasa wanafanya kazi tu kama inavyohitajika na sio zaidi.Hawana tena ari ya kujitolea zaidi .

Wanafanya kwa kadiri wasipate kukaripiwa na si zaidi.Na vipi dunia ilivyobadilika ? kizazi kilichopita tu kikisifiwa kuwa wajerumani ni wachapa kazi-urithi wa enzi za Pressia za kutimiza wajibu wako na ubinafsi ukiweka nyuma.Enzi hiyo yabainika imepita.Dhamana na wajibu hakuna tena......"

 • Tarehe 15.01.2009
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GYrh
 • Tarehe 15.01.2009
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GYrh
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com