1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliokufa yaongezeka Lagos-Nigeria

14 Machi 2019

Waokozi nchini Nigeria wamejaribu kutafuta wanafunzi baada ya jengo la ghorofa kuporomoka nchini humo alisema msemaji wa masuala ya maafa .

https://p.dw.com/p/3F19n
Nigeria - dreistöckiges Gebäude in Lagos eingestürzt
Picha: picture-alliance/AP Photo

 

 

Mamlaka nchini humo imesema  hakuna taarifa sahihi iliyotolewa kwamba ni idadi ya watu wangapi wamefariki baada ya jengo hilo lenye shule iliyopo ghorofa ya juu kuporomoka siku ya jumatano.

Mwili mwingine umeonekana kwenye vifusi vya jengo la shule lililoporomoka katika Mji ,Mkuu wa Nigeria Lagos , waokoaji wamesema hii leo na kufanya idadi ya vifo kuongezeka na kufikia tisa.

`´Tumefanya kazi ya uokoaji usiku kucha na tumepata mwili mmoja´´alisema Mratibu wa Kusini Magharibi kutoka Shirika la kupambana na majanga ya kitaifa (NEMA) Ibrahim Farinloye.

Jengo hilo lilianguka katika makazi yenye watu wengi kwa ghafla bila ya ishara yeyote Mjini Lagos .

Wakazi wa Lagos, zima moto pamoja na wafanyakazi wa huduma ya kwanza waliingia katika jengo hilo kutoa msaada wa kutafuta watu waliokwama kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka.

Jamii inasubiri kuona kama kuna manusura
Jamii inasubiri kuona kama kuna manusuraPicha: picture-alliance/AP Photo

Juhudi za uokozi zimesitishwa

Inasemekana watu 37 waliokolewa wakiwa hai alisema Mratibu wa Shirika la kupambana na majanga Ibrahim Farinloye.

Gavana wa mji wa Lagos Akinwunmi Ambode amesema ilitolewa tahadhari ya kutotumika kwa jengo hilo lakini shule ya chekechea na shule ya msingi ziliendelea kuendesha shughuli zake katika moja ya sehemu ya jengo hilo kinyume na taratibu.

Katika harakati za uokozi kulionekana mabegi ya watoto , michezo ya watoto pamoja na nguo zikiwa katika vifusi baada ya kufanywa usafi katika eneo hilo .

Muuza duka wa eneo hilo Adeniyi Afolabi alitaja jina la shule hiyo Ohen Nursery na Primary na kusema kabla ya jengo kuanguka idadi ilionyesha kulikuwa na wanafunzi 144 waliofika shuleni siku ya jumatano kabla jengo kuporomoka kwa ghafla.

Mmoja ya mkazi wa eneo hilo Zion Munachi alithibitisha majina na idadi ya wanafunzi waliokuwepo shuleni siku hiyo, wote kwa pamoja walisema sio watoto wote walikua shuleni kutokana na ratiba ya michezo siku hiyo.

Joshua Yang , kutoka huduma ya zimamoto mjini Lagos amesema eneo la chekechea limesafishwa vizuri .

Waokozi wanaendelea kufukua vifusi kuwatafuta manusura
Waokozi wanaendelea kufukua vifusi kuwatafuta manusuraPicha: picture-alliance/AP Photo/S. Alamba

´´Hakuna watu waliobakia katika vifusi ´´aliiambia televisheni ya TVC mjini humo.

Kuanguka kwa majengo nchini Nigeria si jambo geni limezoeleka ambapo sheria za ujenzi hazifwatiliwi kwa ukaribu na hii ndio imekua athari kubwa nchini humo. September mwaka 2014 watu 116 walifariki na 84 kati ya idadi hiyo walikua ni raia wa Afrika Kusini baada ya nyumba yakulala wageni yenye ghorofa sita kuporomoka na kuangukia katika kanisa la mtabiri TB Joshua.

Uchunguzi ulipofanyika uligundua kwamba kuna baadhi ya ngazi ziliongezwa bila kufuata utaratibu wala mpangilio wowote.

Mwaka 2016 watu 60 waliuawa baada ya paa la jengo kuanguka katika kanisa huko Uyo mji mkuu wa Akwa ibom state kusini mwa Nigeria.

Shughuli za uokoaji zimesitishwa hivi sasa baada ya eneo hilo kusafishwa hii leo na hakuna kilichopatikana zaidi ya mtu mmoja ambae alikutwa akiwa amefariki.

 

Mwandishi : Zainab Chondo

Mhariri:   Yusuf Saumu