1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiTunisia

Idadi ya wahamiaji wanaojaribu kuelekea Ulaya yaongezeka

13 Mei 2024

Tunisia imeripoti ongezeko la asilimia 22.5 ya wahamiaji waliozuiliwa aidha wakiwa ufuoni au kuokolewa baharini wakati wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania kutoka nchini Tunisia kuelekea Italia.

https://p.dw.com/p/4flgU
Wahamiaji ambao wanaojaribu kuvuka kuelekea Italia wamezuiliwa na Walinzi wa Kitaifa  kwenye pwani ya Sfax nchini Tunisia.
Wahamiaji ambao wanaojaribu kuvuka kuelekea Italia wamezuiliwa na Walinzi wa Kitaifa kwenye pwani ya Sfax nchini Tunisia.Picha: Hasan Mrad/ZUMA Press/picture alliance

Walinzi wa kitaifa wa Tunisia wameeleza kuwa zaidi ya watu 21,000 wamezuiwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu 2024.

Taarifa ya walinzi hao wa kitaifa imeendelea kueleza kuwa watu 21,545 walizuiwa kati ya Januari mosi na Aprili 30, tofauti na watu 17,576 katika kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Soma pia: Italia yataka Umoja wa Ulaya kuisaidia Tunisia

Tunisia na nchi jirani ya Libya zimekuwa vituo muhimu vinavyotumiwa na wahamiaji kutoka nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ambao wanafanya safari za hatari baharini kwa nia ya kutafuta maisha mazuri barani Ulaya.

Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la kimataifa la uhamiaji la Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa katika muda wa muongo mmoja uliopita, zaidi ya wahamiaji 27,000 wamepoteza maisha wakijaribu kuelekea Ulaya kwa kutumia boti huku zaidi ya 3,000 kati yao wakifariki mwaka uliopita pekee.