Hummels ataka kurejea Bayern | Michezo | DW | 29.04.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Hummels ataka kurejea Bayern

Beki wa Borussia Dortmund Mats Hummels ameiambia klabu yake kuwa anataka kujiunga na viongozi wa ligi ya kandanda ya Ujerumani – Bundesliga, Bayern Munich baada ya kukamilika msimu huu

Mapema wiki hii, mwenekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alifichua kuwa klabu hiyo ilikuwa tayari inafanya mazungumzo na nahodha huyo wa Dortmund kuhusu uhamisho.

Dortmund imethibitisha katika taarifa kuwa mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ujurumani mwenye umri wa miaka 27, ambaye ana mkataba hadi Juni 2017 amewasilisha ombi rasmi la kutaka kuondoka. Kwa sasa Bayern haijatoa ofa na kuwa mchezaji huyo ataweza kuondoka tu ikiwa kwa kutolewa kiasi cha pesa kitakachokubaliwa. Hummels atajiunga na Mario Goetze aliyeondoka mwaka wa 2013 kwa kiasi cha euro milioni 37 na mshambuliaji Robert Lewandoswki aliyesaini mwaka wa 2014.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Iddi Sessanga