1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW yaonya ongezeko la ukandamizaji wanaharakati Thailand

16 Mei 2024

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema hivi leo kuwa wanaharakati na wapinzani wanaotafuta hifadhi nchini Thailand wamekuwa wakinyanyaswa.

https://p.dw.com/p/4fuM9
Wanaharakati wa Thailand
Wanaharakati wa Thailand Picha: Sakchai Lalit/AP

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema hivi leo kuwa wanaharakati na wapinzani wanaotafuta hifadhi nchini Thailand wamekuwa wakinyanyaswa, kufuatiliwa na kufanyiwa ukatili na mara nyingi kwa ushirikiano na mamlaka ya Thailand.

Soma: Waziri Mkuu mpya wa Thailand aapishwa na kuahidi mabadiliko

HRW imeeleza kwamba katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukandamizaji dhidi ya raia wa kigeni walioomba hifadhi nchini humo.

Thailand imekosolewa pia kwa kuwakabidhi watu hao kwa mataifa yao kwa lengo la kukabidhiwa pia wakosoaji wa Thailand wanaoishi nje ya nchi. Mataifa yaliyohusishwa na hatua hizo ni pamoja na China, Bahrain na nchi wanachama wa Jumuiya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN).