HRW: Mashambulizi yasababisha vifo vya watu wengi katika siku za mwanzo za vita Tigray | Matukio ya Afrika | DW | 11.02.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

HRW: Mashambulizi yasababisha vifo vya watu wengi katika siku za mwanzo za vita Tigray

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la HRW limesema wanajeshi wa Ethiopia walitumia wiki za mwanzo za mzozo wa jimbo la Tigray kuyashambulia kwa silaha nzito maeneo yenye watu wengi na kusababisha vifo vya raia 83.

Kulingana na ripoti ya shirika hilo vikosi vya serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed vilizilenga nyumba za makaazi, hospitali, shule na masoko katika maeneo ya mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekele na miji mingine ya Shire na Humera. Human Rights Watch imeutaka Umoja wa Mataifa kuchunguza iwapo sheria za vita zilikiukwa kutokana na taarifa kwamba wanajeshi walifanya mshambulizi bila kubagua na kusababsiha vifo vya watu na kuharibu mali. Operesheni ya kijeshi dhidi ya jimbo la Tigray ilitangazwa Novemba mwaka uliopita na Waziri Mkuu Abiy aliyewatuhumu viongozi wa chama cha TPLF kilichokuwa kinaongoza eneo hilo kwa uhaini baada ya kuzishambulia kambi za jeshi la taifa.