1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hospitali ya Kisumu yakabiliwa na uhaba oksijeni

16 Aprili 2021

Hospitali za umma katika eneo la Kisumu nchini Kenya zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa hewa muhimu ya Oxijen inayotumiwa na wagonjwa, hali inayosababisha kudorora kwa huduma za matibabu.

https://p.dw.com/p/3s8Ak
Coronavirus Südafrika | Klinik mit Covid-19 Station
Picha: RODGER BOSCH/AFP

Afisa mkuu mtendaji wa hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga, ambayo ndiyo inayotegemewa na idadi ya watu zaidi ya milioni 5 katika ukanda wa Magharibi mwa Kenya Dkt.

George Rae anasema tatizo hilo limetokana  na upungufu wa uzalishaji wa oxijen kipindi hichi cha janga la korona ambapo hewa hii imekuwa adimu kutokana na ongezeko la mahitaji nchini humo.

Kwa sasa kiwango kidogo kinachotolewa kinatolewa tu kwa mahitaji ya dharura. Gavana wa jimbo la Kisumu Prof. Peter Anyang Nyong'o amesema tayari wameanza mradi wa kituo cha uzalishaji hewa ya oxijen ya mitungi katika hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga, ili kuzuia upungufu katika siku za usoni.

Hali hii inajiri takriban wiki mbili tangu serikali kuu kupitia kwa waziri wa afya Mutahi Kagwe kukiri kuwepo upungufu wa hewa ya oxijen na uhaba wa mitungi nchini humo.