1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Iran | Kabinettssitzung in Teheran | Präsident Hassan Rouhani
Picha: Iranian Presidency/dpa/picture alliance

Hofu yazuka baada ya Iran kurutubisha madini ya urani

14 Aprili 2021

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimeonesha wasiwasi wao kufuatia uamuzi wa hivi karibuni wa Iran wa kutangaza kurutubisha madini ya Urani kwa asilimia 60

https://p.dw.com/p/3s0t9

Katika taarifa ya pamoja, nchi hizo zenye uchumi mkubwa barani Ulaya zimesema hicho ni kiwango kikubwa kuelekea utengenezaji wa silaha za nyuklia, na kwamba Iran haina sababu ya kufanya hivyo.

Hata hivyo, kulingana na msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran, madini yaliyorutubishwa yatatumika kwa ajili ya matibabu.

soma zaidi: Iran yaonya hujuma zinaathiri mazungumzo ya Vienna

Wakati huo huo, Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema ana matumaini ya kuendelea tena na mazungumzo ya mkataba wa nyuklia wa Vienna wa mwaka 2015, licha ya kutangaza kuwa nchi yake itaendelea na mipango ya kurutubisha madini ya Uranium.

Rouhani ameongeza kusema, mara tu baada ya nchi zilizosaini mkataba huo zitakapotekeleza makubaliano yao na pia Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya Iran, basi Iran itaendelea tena na mazungumzo hayo.