Kenya ni moja ya mataifa yanayoshuhudia ongezeko la idadi ya watu kwa kasi zaidi barani Afrika. Idadi ya watu inapoongezeka, taka pia huongezeka. Wadau katika maswala ya mazingira wanahimiza mfumo wa kupunguza, kusindika na kurejeleza matumizi ya taka, kwa malengo ya kusafisha na kuhifadhi mazingira.