Hamilton atetea taji la ubingwa wa dunia F1 | Michezo | DW | 26.10.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Hamilton atetea taji la ubingwa wa dunia F1

Lewis Hamilton amejiunga katika kundi la kifahari la mabingwa mara tatu wa ulimwengu katika mashindano ya Formula One baada ya kushinda mbio za kusisimua za US Grand Prix

Lewis alimaliza mashindano hayo mbele ya mwenzake wa timu ya Mercedes Nico Rosberg ambaye alikuwa akiongoza kwa wakati mmoja kabla ya kutokea kosa lililomwezesha Hamilton kumpiku.

Hamilton ndiye Muingereza wa kwanza kushinda mfululizo mataji ya ulimwengu ya Formula One na kuifikia rekodi iliyowekwa na dereva nguli Ayrton Senna aliyefariki dunia mwaka wa 1994. Sebastian Vettel wa timu ya Ferrari alimaliza katika nafasi ya tatu.

Hata hivyo Rosberg alikasirishwa na matokeo hayo akimlaumu Hamilton kwa kukosa nidhamu mwanzoni mwa mashindano ya jana. Madereva hao wawili walikaribiana sana nusra magari yao yagongane.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mharrii: Iddi Sessanga