1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya usalama DRC yaendelea kudorora

John Kanyunyu DW Beni.28 Novemba 2019

Watu 5 wameuawa leo kufuatia shambulizi la wapiganaji wa Maimai katika kituo cha WHO mkoani Ituri. Hapo jana watu wengine 19 waliuawa mkoa wa Kivu kaskazini.

https://p.dw.com/p/3Ts10
Demokratische Republik Kongo | Überfall auf UN-Lager in Beni
Picha: picture-alliance/dpa/0AP Photo/A.-H. K. Maliro

Watu watano wanaripotiwa kuuwawa  leo baada  ya wapiganaji wa maimai kushambulia kituo cha shirika la afya ulimwenguni WHO katika mji mdogo wa Biakato mkoani Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Na katika mkoa wa Kivu ya kaskazini, waasi kutoka Uganda ADF nao waliwauwa jana watu kumi na tisa katika kijiji cha Maleki katika wilaya ya Beni.

Akizungumza na DW kwa njia ya simu, naibu mwenyekiti wa baraza la vijana katika mji mdogo wa Biakato Kabuyaya Saidi alisema, kuwa wapiganaji wa maimai waliushambulia mji huo saa sita za usiku na kurudi tena kushambulia Biakato saa kumi na moja alfajiri ya leo.

Shambulio la usiku wa kuamkia leo katika mji mdogo wa Biakato ni la pili kutokea katika mji huo,wapiganaji wa maimai wakiwa wanajificha katika viunga vya mji huo, na wengi wao wakiwa nia yao ni kuwashambulia watabibu katika makabiliano dhidi ya homa ya EBOLA.

Baadhi ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO vikifanya doria Congo. (Picha ya maktaba)
Baadhi ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO vikifanya doria Congo. (Picha ya maktaba)Picha: Reuters/File Photo/O. Oleksandr

Aidha shambulio hili linatokea, baada ya shirika la afya Ulimwenguni WHO, kuwahamisha kutoka Beni baadhi ya wafanyakazi wake, kutokana na hali mbaya ya usalama katika eneo hili, hasa maandamano ya karibia kila siku katika mji wa Beni, pale waandamanaji wakiomba ujumbe wa Umoja wa mataifa wa kulinda amani, Monusco, kuondoka Beni.

Nao wadadisi wa masuala ya afya wanadhani kuwa, shambulizi la leo huenda likaathiri mpango mzima wakupambana na EBOLA,na idadi ya maambukizi mapya huenda ikaonezeka munamo siku za usoni.

Na huko hayo yakiwa namna hiyo, waasi kutoka Uganda ADF, waliwauwa watu kumi na tisa jana katika kijiji cha Maleki, kilomita tisa magharibi mwa mji mdogo wa Oicha.

Mauwaji hayo yakiwa ni moja wapo ya mrorongo wa mauwaji katika eneo hili, yanalaaniwa na mashirika ya kiraia, yanayowaomba wanajeshi wa serikali kufanya juu chini, ilikuwalindia usalama wakaazi katika viunga vya maeneo yanayoshuhudia mapigano.

Akizungumza na DW, mkuu wa wilaya ya Beni Donant Kibwana, akiwa anaomboleza na familia zilizopigwa msiba, anawaomba viongozi wa jeshi katika operesheni dhidi ya ADF,kufanya juu chini ilikuhakikisha kuwa ADF hawauwi wakaazi, wakati vita vikiendelea.

Mauaji ya jana katika kijiji cha Maleki, yamepelekea idadi ya watu waliouawa na ADF kuongozeka na kuwa tisini na tisa, tangu yalipoanza mauwaji hayo, novemba tano.