1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya Kenya yatia wasiwasi

28 Machi 2023

Mchambuzi Martib Oloo anaelezea jinsi hali ya wasiwasi ilivyotanda katika mtaa wa Kibra jijini Nairobi kufuatia uharibifu uliofanyika wakati wa maandamano ya siku ya Jumatatu (Machi 27) ya kuishinikiza serikali kupunguza gharama ya maisha.

https://p.dw.com/p/4PNut

Inaelezwa kuwa vibanda vya biashara na baadhi ya maeneo ya ibada ukiwemo msikiti mmoja na kanisa la PCEA yamechomwa moto na magenge ya wahalifu.

Kwengineko katika Kaunti ya Kiambu, magenge ya wahalifu walivamia shamba la Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta na kuiba mifugo.

Je, maandamano ya jana Jumatatu yamekuwa na athari ya kiasi gani nchini Kenya? Babu Abdallah anazungunza na mchambuzi wa siasa akiwa mjini Nairobi, Martin Oloo.