1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Haiti yarefusha hali ya hatari kwa mwezi mmoja zaidi

Sylvia Mwehozi
8 Machi 2024

Serikali nchini Haiti imetangaza kurefusha hali ya hatari kwa mwezi mmoja zaidi, haswa upande wa magharibi mwa nchi, unaojumuisha mji mkuu wa Port-au-Prince.

https://p.dw.com/p/4dI5t
Haiti -Port-au-Prince
Raia akipita kando ya mwanajeshi aliyeko kwenye operesheini ya magenge ya wahalifuPicha: Odelyn Joseph/AP/picture alliance

Serikali nchini Haiti imetangaza kurefusha hali ya hatari kwa mwezi mmoja zaidi, haswa upande wa magharibi mwa nchi, unaojumuisha mji mkuu wa Port-au-Prince.

Magenge ya wahalifu yaliyojihami kwa silahayalianzisha mashambulizi mapema wiki iliyopita, na kuilenga miundombinu muhimu ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege, vituo vya polisi na kuvunja magereza.

Mamlaka pia zimelazimika kuifunga bandari kuu, zikitaja hujma zinazofuatia siku kadhaa za ghasia mbaya za magenge ya wahalifu. Ghasia hizo zimeitumbukiza Haiti katika machafuko na kusababisha waziri mkuu kushindwa kurejea nchini humo.Watu 42 wafariki Haiti kwenye maporomoko na mafurukoUN: Yatoa wito wa kupelekwa kikosi cha kimataifa nchini Haiti

Wakati hali ikiwa bado ni tete, ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeonya kwamba mfumo wa afya unakaribia kushindwa kufanya kazi, wakati vituo vingi vikiwa vimefungwa au kupunguzwa huduma na upungufu wa madawa na wafanyakazi.