Guterres ataka uchaguzi Sudan Kusini kufanyika
18 Aprili 2024Katika ripoti yake iliyochapishwa siku ya Jumatano (Oktoba 17), Guterres aliandika kwamba, kwa maoni yake, vyama lazima vijitolee kuchukua hatua za haraka kupata taasisi muhimu za kuendesha uchaguzi huru wa amani, wa haki na wa kuaminika.
Soma zaidi: Juhudi za amani Sudan Kusini zasambaratika tena
Sudan Kusini haijafanya uchaguzi tangu ilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa Sudan mwaka 2011 na taifa hilo linakumbwa na ghasia, umaskini na majanga ya asili.
Mipango ya uchaguzi imevurugwa na mabishano makali kati ya Rais Salva Kiir na hasimu wake mkuu, Makamu wa Rais Riek Machar.
Waangalizi wa kimataifa wana mashaka iwapo muda mpya uliowekwa kufanyika uchaguzi wa Disemba mwaka huu utaheshimiwa, kwani Kiir na Machar bado hawajafikia muafaka wa kuandaa uchaguzi huo.