1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres: Kupunguzwa kwa bajeti ya misaada kumeleta maafa

23 Septemba 2025

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hii leo kwamba kupunguzwa kwa bajeti ya misaada kumesababisha uharibifu mkubwa.

https://p.dw.com/p/50yEe
USA New York 2025 | Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hii leo kwamba kupunguzwa kwa bajeti ya misaada kumesababisha uharibifu mkubwa. Guterres ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kutoa taswira mbaya ya utaratibu wa dunia. Guterres ameongeza kuwa, hatua hiyo imekuwa kama adhabu ya kifo kwa watu wengi bila ya kutaja Marekani ambayo ndio mhusika mkubwa wa kupunguzwa misaada.

Katika hotuba iliyojaa hali ya kutisha, Guterres ameashiria kuwepo kwa hali mbaya ya migogoro katika idadi inayoongezeka ya nchi na kuonya juu ya hatari ya kuenea kwa silaha za nyuklia. Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa anasema migogoro mingi inaendelea bila kudhibitiwa, hali ya watu kufanya makosa bila kuadhibiwa, na sheria kutoheshimiwa.