1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Greenpeace - Shirika la kimataifa la kutetetea mazingira

Greenpeace ni shirika la kimataifa linalohusika na masuala ya mazingira. Shirika hili ilitokana na vuguvugu la kupigania amani duniani pamoja na kupinga utengenezaji wa silaha za kinyuklia katika miaka ya 1970.

Shirika la Greenpeace lina ofisi zake katika nchi 40 tofauti, na bodi yake ya uratibu ipo nchini Uholanzi. Shirika hili mara kwa mara hugonga vichwa vya habari kutokana na kampeni zake duniani kote zinazohusiana na masuala ya; ongezeko la joto duniani, ukataji ovyo wa miti, uvuvi wa kupita kiasi, silaha za kinyuklia na mengine mengi. Shirika la Greenpeace halipokei ufadhili wa aina yoyote kutoka katika serikali, mashirika au vyama vya kisiasa.