Goetze huenda akarejea uwanjani Februari | Michezo | DW | 08.01.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Goetze huenda akarejea uwanjani Februari

Mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich bado tu watazikosa huduma za kiungo wa Ujerumani Mario Goetze wakati sehemu ya pili ya msimu wa Bundesliga itakaporejea baadaye mwezi huu.

Goetze anasema analenga kurejea uwanjani mwezi Februari wakati akiendelea kupona kupona baada ya kuumia katikati ya Oktoba mwaka jana. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 bado hajaanza kufanya mazoezi kamili licha ya kuwa anafanyiwa mazoezi ya kibinafsi mjini Doha, Qatar.

Sehemu ya pili ya msimu itakuwa awamu muhimu kwa Goetze aliyejiunga na Bayern mwaka wa 2013 na ana mkataba hadi mwishoni mwa msimu wa 2016-17. Kwa mujibu wa gazeti la michezo la Bild, Liverpool chini ya kocha Juergen Klopp inaonyesha nia ya kumtaka kiungo huyo.

Goetze alicheza chini ya Klopp katika Borussia Dortmund kati ya 1009 na 2013. Bayern, ambao wako kileleni mwa msimamo wa Bundesliga mbele ya Borussia Dortmund na pengo al pointi nane, watakutana na Hamburg Januari 22 katika mpambano wa Ijumaa jioni wakati Bundesliga itakapoejea.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Iddi Sessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com