Ghasia zatanda Pakistan | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 29.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Ghasia zatanda Pakistan

---

ISLAMABAD

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan ametoa amri kwa maafisa wakuu wa usalama kuchukua hatua kali dhidi ya waandamanaji nchini humo kufuatia mauaji ya kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kituo cha televisheni ya taifa rais Musharraf ametoa agizo hilo katika mkutano na maafisa wa ngazi ya juu akiwemo kiongozi wa jeshi na maafisa wengine wa usalama pamoja na waziri mkuu wa muda.Hali ya wasiwasi imetanda nchini Pakistan huku maduka vituo vya kuuza mafuta na biashara nyingine zikifungwa.

Watu 38 wameuwawa kufuatia ghasia zinazoendelea nchini humo.Rais Musharraf ametoa mwito kwa wananchi wa Pakistan wazingatie sheria akisema taifa zima linasikitika juu ya mauaji ya Bhutto.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com