1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroGhana

Ghana: Raia wetu 55 waliuawa katika vita nchini Ukraine

28 Februari 2026

Serikali ya Ghana imesema raia wake wapatao 55 wameripotiwa kuuawa katika vita nchini Ukraine, huku ikiahidi msako mkali dhidi ya wanaohusika na mipango haramu ya kuwarubuni na kuwasafirisha raia wa nchi hiyo hadi urusi.

https://p.dw.com/p/59ZrJ
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Samuel Okudzeto Ablakwa akiwa na mwenzake wa Ukraine Andrii Sybiha mjini Kiev
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Samuel Okudzeto Ablakwa akiwa na mwenzake wa Ukraine Andrii Sybiha mjini KievPicha: Tetiana Dzhafarova/AFP/Getty Images

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Samuel Okudzeto Ablakwa alifanya ziara wiki hii mjini Kyiv kujadili kuhusu hatima ya Waghana wawili waliokamatwa kwenye mstari wa mbele wa vita.

Hii ni idadi inayoongezeka katika miezi ya hivi karibuni ambapo nchi kadhaa za Afrika ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Afrika Kusini, na Gambia, zimekuwa zikigundua kuwa raia wao walidanganywa kupewa ajira na mishahara minono na badala yake wakajikuta wamesajiliwa katika jeshi la Urusi, huku wengi wakiuawa au kukamatwa kwenye uwanja wa vita.