Ghana kuumana na Libya katika fainali ya CHAN | Michezo | DW | 31.01.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ghana kuumana na Libya katika fainali ya CHAN

Pazia la dimba la Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka katika ligi za nyumbani – CHAN zinateremshwa Jumamosi (01.02.2014) ambapo Ghana na Libya zitashuka dimbani kupambana katika fainali.

Ghana na Libya zilijikatia tikiti ya kucheza katika fainali baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali kwa mikwaju ya penalty baada ya mechi kumalizika sifuri kwa sifuri katika muda wa kawaida na wa ziada.

Ghana inalenga kusahau masaibu yaliyowakumba katika dimba la 2009, waliposhindwa kwenye fainali na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ghana ilifungwa magoli mawili kwa sifuri katika dimba hilo lililochezwa nchini Cote d'Ivoire.

The Black Stars waliwaduwaza Nigeria kwa kusukuma wavuni penalty nne kwa moja. Libya nao walifuzu baada ya kuwazaba Zimbabwe penalty tano kwa nne. Mlinda lango wa Libya Mohamed Abdaula alikuwa nyota wa timu yake, alipookoa penalty ya mwisho ya Zimbabwe kabla ya kufunga penalty yake mwenyewe ambayo ilikuwa ya ushindi.

Mwandishi. Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu