Gabon: Mitandao ya kijamii imefungwa kwa muda usiojulikana
18 Februari 2026
Haya yanajiri huko wakosoaji wakimtuhumu rais wa taifa hilo Gen. Brice Clotaire Oligui Nguema kwa kuwakandamiza wapinzani wake.
Wizara ya mawasiliano imesema imegundua kuwa katika mitandao hiyo ya kijamii kuna uwanja mpana wa kupeleka maudhui ya yasiyofaa, ya kupotosha, ya chuki na yasio ya lugha nzuri yanayoudhoofisha utu wa binaadamu kutia doa taasisi za taifa na usalama wa taifa kwa ujumla.
Wizara hiyo imesema makosa yanayofanyika mitandaoni yanaweza kubeba adhabu chini ya sheria ya kitaifa na kimataifa na pia chini ya sera zilizopitishwana za mitandaoni.
Mitandao ya kijamii kama Meta Tik Tok na Whats up ndizo zilizoathirika zaidi na ndizo zinazotumika kwa wingi na raia wa Gabon hasa Vijana. Simu pia zinazopigwa kupitia whats up pia zilikuwa na changamoto kubwa hii leo Jumatano.