1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Frankfurt na Freiburg zatekwa sare

23 Septemba 2013

Timu zinazocheza katika Europa League Eintracht Frankfurt na Freiburg zilitekwa kwa sare ya goli moja kwa moja dhidi ya Hertha Berlin na VfB Stuttgart katika mechi za Bundesliga

https://p.dw.com/p/19mRl
Ilikuwa ni hadithi ya kukosa kufunga nafasi za wazi katika mechi ya SC Freiburg - Hertha BSC Berlin
Ilikuwa ni hadithi ya kukosa kufunga nafasi za wazi katika mechi ya SC Freiburg - Hertha BSC BerlinPicha: picture-alliance/dpa

Mshambuliaji wa Stuttgart Vedad Ibisevic alifyatua kombora la penalti juu ya lango na kupoteza penalti ambayo iliwafanya Frankfurt kuponea. Matokeo hayo sasa yamewaweka Hertha Berlin katika nafasi ya nane na pointi nane, huku Stuttgart na Frankfurt zikiwa katika nafasi ya 12 na 13 na pointi saba kila mmoja. Freiburg inayumbayumba chini ya ligi na pointi tatu pekee. Mlinda lango wa Stuttgart Sven Ulreich anaitahmini sare hiyo dhidi ya Frankfurt.

Borussia Dortmund na Bayern Munich zinashikilia uongozi wa msimamo wa ligi zikiwa na pointi 16 kila mmoja, ijapokuwa BVB wana faida ya mabao 16 tofauti na Bayern ambao wamefunga 13. Bayern Munich iliwasambaratisha Schalke kwa kuwafunga mabao manne kwa sifuri katika kile kocha „Pep Guardiola alikitaja kuwa ni mchezo wao mzuri zaidi katika Bundesliga msimu huu“. Beki wa Bayern Jerome Boateng ambaye alicheza dhidi ya kakake Kevin Prince Boateng, amesema matokeo hayo yanaonesha kuwa wana ari ya kuendelea kufanya vyema

Dortmund iliangusha pointi zake za kwanza msimu huu baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja dhidi ya washika mkia Nuremberg siku ya Jumamosi. Jurgen Klopp ni kocha wa BVB. Bayer Leverkusen iliendeleza matokeo yake bora baada ya kuichabanga Mainz 05 mabao manne kwa moja na kusalia katika nafasi ya tatu na pointi 15.

Borussia Dortmund walikabwa na 1. FC Nürnberg
Borussia Dortmund walikabwa na 1. FC NürnbergPicha: picture-alliance/dpa

Kombe la DFB

Ikiwa ni siku kumi tu baada ya matamshi yaliyozusha utata ya mkurugenzi wa spoti wa Bayern Munich Mattias Sammer, washindi hao wa mataji matatu msimu uliopita, wanawaalika tena Hanover Jumatano wiki hii katika mechu ya duru ya pili ya kombe la Shirikisho.

Sammer alisema baada ya Bayern kuwashinda Hanover mabao mawili kwa sifuri kuwa timu inaonekuwa kuwa yenye uchovu, na isiyokuwa na hamu. Matamshi hayo hayakuchukuliwa vyema na Rais Uli Hoeness na mwenyekiti Karl-Heinz Rummenige, lakini ukweli wa mambo ni kwamba sasa Bayern wanaendelea kushinda mechi zao mfulululizo. Wakati Bayern wakicheza dhidi ya Hanover Jumatano, nao Dortmund watacheza kesho Jumanne dhidi ya 1860 Munich. Katika mechi nyingine zitakazochezwa keshoa na Jumatano za awamu ya 16 ya kombe la shirikisho, SC Freiburg italenga kulipiza kisasi kichapo cha nusu fainali msimu uliopita itakapowaalika VfB Stuttgart. SV Hamburg itawaalika viongozi wa daraja ya pili Greuther Fuerth, wakati Bayer Leverkusen ikichuana na Arminia Bielefeld nayo Schalke ikifunga kazi dhidi ya timu ya daraja ya tatu Darmstadt.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters

Mhariri: Yusuf Saumu