Florent Malouda asajiliwa na klabu ya Misri | Michezo | DW | 29.01.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Florent Malouda asajiliwa na klabu ya Misri

Klabu ya Misri Wadi Degla imemsajili aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa na Chelsea Florent Malouda

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 amejiunga kutoka klabu ya Delhi Dynamos nchini India ambako amekuwa akisakata soka lake tangu mwaka 2015 mwezi Agosti.

Ameandikisha mkataba hadi mwisho wa msimu na anajiunga na mchezaji mwenzake wa Ufaransa Patrice Carteron ambaye alikuwa mkufunzi wa kilabu hiyo mapema mwezi Januari.

Malouda ambaye ameichezea Chelsea kutoka mwaka 2007 hadi 2013, aliichezea Ufaransa mara 80 na kufunga mbao tisa ya kimataifa.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA/reuters
Mhariri: Daniel Gakuba

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com