F1: Vettel ashinda Monaco | Michezo | DW | 29.05.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

F1: Vettel ashinda Monaco

Katika mashindano ya magari ya formula one, Sebastian Vettel alikuwa na wikendi yenye furaha baada ya kushinda mbio za mkondo wa Monaco. Anaonoza ubingwa wa dunia akiwa na pengo la pointi 25 mbele ya Lewis Hamilton

Ikiwa ni mikondo sita baada ya kuanza msimu mpya, dereva huyo Mjerumani wa timu ya Ferrari anaongoza msururu wa ubingwa wa dunia akiwa na pengo la pointi 25 mbele ya Muingereza Lewis Hamilton.

Dereva mwenza wa Vettel wa timu ya Ferrari Kimi Raikkonen alimaliza wa pili wakati Daniel Ricciardo wa Red Bull akipanda jukwaani katika nafasi ya tatu. Ulikuwa ushindi wa tatu wa Vettel msimu huu na wa kwanza kwa Ferrari katika mkondo wa Monaco tangu Michael Schumacher aliposhinda mwaka wa 2001. Hamilton alimaliza katika nafasi ya saba nyuma ya dereva mwenza wa Mercedes Valtteri Bottas aliyemaliza wa nne.

Mwandish: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com