1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

F1: Verstappen ampiku Hamilton katika mashindano ya Italia

Bruce Amani
19 Aprili 2021

Dereva wa timu ya Red Bull Max Verstappen alishinda mashindano ya Emilia Romagna Grand Prix nchini Italia yaliyokumbwa na vurugu chungu nzima kutokana na mvua.

https://p.dw.com/p/3sEI0
Formel 1 | Grand Prix Emilia Romagna | Verstappen
Picha: Jennifer Lorenzini/REUTERS

Max Verstappen alishinda mashindano ya Emilia Romagna Grand Prix nchini Italia yaliyokumbwa na vurugu chungu nzima kutokana na mvua. Bingwa mara saba wa dunia katika Formula One Lewis Hamilton wa timu ya Mercedes alijikwamua baada ya kufanya makosa ya nadra katika mashindano hayo na akamaliza wa pili.

Muingereza Lando Norris wa timu ya McLaren alikamata nafasi ya tatu mbele ya Mfaransa Charles Leclarc wa Ferrari aliyeridhika na nafasi ya nne.

Matokeo hayo ya mkondo wa pili wa wa msimu yamedhihirisha nafasi ya Verstappen kuwa kizingiti kikubwa kwa jaribio la Hamilton la kubeba taji la nane duniani.

AFP/DPA/AP/Reuters