F1: Hamilton atawala katika mashindano ya Uingereza | Michezo | DW | 15.07.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

F1: Hamilton atawala katika mashindano ya Uingereza

Bingwawa dunia Lewis Hamilton aliufurahisha umati mkubwa wa mashabiki wa nyumbani kwa kuweka rekodi ya ushindi wa sita ya taaluma yake katika mashindano ya Grand Prix ya nchini Uingereza

Hamilton alishinda mbio hizo zilizojaa vituko, kwa kumpiku dereva mwenzake wa timu ya Mercedes aliyeanza katika nafasi ya kwanza Valtteri Bottas baada ya kuchukua uongozi wakati gari la usalama lilipotumika katika mzunguko wa 20.

Dereva wa Ferrari Charles Leclerc alimaliza katika nafasi ya tatu baada ya Sebastian Vettel na gari lake la Ferrari kumgonga dereva wa Red Bull Max Verstappen kwa upande wa nyuma katika mapambano ya kutafuta nafasi kwenye jukwaa la washindi.

Hamilton sasa ameshinda misimu saba na jumla ya mbio 80, ikiwa ni pungufu ya 11 kuifikia rekodi ya Mjerumani Michael Schumacher ya mashindano 91.